Pichaz za maeneo mengine alikofika Rais Obama kwenye nchi 50 alizotembelea…DUNIANI
Safari ya Rais Obama ndani ya Kenya imeweka rekodi ambayo sikuwa nafahamu, kumbe kwa kipindi ambacho Rais Obama amekaa madarakani ambacho ni kama miaka saba hivi anakuwa ametembelea jumla ya nchi 50 nje ya Marekani.
Mmoja ya Wapigapicha wa White House, Pete Souza kazitoa picha 50 ambazo hazikuwahi kuonekana mahali popote !!
Hapa ziko pichaz 12 kati ya hizo mtu wangu.
Aliwahi kufika Msikiti wa Istiqlal uliopo Jakarta, Indonesia… Katikati yuko Imam Ali Mustafa Yaqub, na pembeni mwenye suti na kilemba ni Michelle Obama… November 2010 alikuwa kwenye Msikiti huo na alifuata taratibu za hapo kwa kuvua viatu yeye pamoja na mkewe.
Kuna wakati alijiachia bila Timu ya Walinzi wake, hii alikuwa anakatisha zake Panama Marekani, April 2015.
Wakati mwingine anaenjoy story na watu wa kawaida kabisa, hapa alikuwa anapiga story na Mkuu wa Wafanyakazi wa Mgahawa wa Esperanza uliopo San Jose del Cabo, Mexico. Hii ilikuwa June 2012.
Kwenye
safari zake alifika na Egypt pia, akatembelea Mapiramidi ambayo nayo
yamo kwenye maajabu ya Duniani.. Hii ilikuwa June 2009.
Aliwahi fika China pia November 2009. Hapa alikuwa kwenye ukuta mkubwa ambao uko pia kwenye Maajabu ya Dunia, ‘the Great Wall of China’.
Muda mwingine wanakuwa na Stori kwenye mazingira tofauti kabisa na Office, hapa alikuwa na Chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel.. Hii ilikuwa Ujerumani June 2015.
Ishu ya kudance ni kawaida tu kwake, hapa alikuwa na Wanafunzi wa Mumbai, India November 2010.. Pembeni ni mkewe, Michelle Obama.
Alitembelea pia haya maeneo ya Kihistoria kwenye nchi ya Burma, utamaduni wao inabidi uwe pekupeku bila viatu.. alivua pia, hii ilikuwa November 2012.
Hakuna maoni