Wema Sepetu Akubali Kushindwa Adai Siasa Bila Kujipanga Utoki... ‘Utakatwa’ tu!
Leo tunaye msanii wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu
ambaye hivi karibuni alithubutu kugombea ubunge kupitia viti maalum mkoani
Singida.
Kwa bahati mbaya kura za msanii huyu hazikutosha.
Mwandishi wetu alionana na mwanadada huyo nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar
na kumpiga maswali 10 mujarabu. Ungana nami…
Ijumaa: Hongera kwa kujitosa kwenye siasa, nini
kilikusukuma kuingia huko?
Wema: Nilikuwa nashauku ya kuwa mheshimiwa, hata
baba yangu aliwahi kuniambia naweza hivyo nikajaribu bahati yangu.
wema (8)Ijumaa: Ukiacha marehemu baba yako, nani
alikupa sapoti kubwa na ukajiona unaweza?Wema: Namshukuru mama yangu, alinipa
sapoti kubwa nikajiona naweza kwani alinitoa hofu niliyokuwa nayo.
Ijumaa: Unadhani kipi kimekuangusha kwenye uchaguzi
ule?
Wema: Uchanga wangu kwenye siasa lakini naamini
muda ulikuwa bado.
Ijumaa: Ingawa hukufanikiwa kupata nafasi ya ubunge
umejifunza nini kupitia siasa?
Wema: Kwa kweli nimejifunza vitu vingi maana
haviendani hata na umri wangu na nimepata ujasiri mkubwa. Kikubwa ukiingia
kwenye siasa ujipange sana.
Ijumaa: Je, kwa hatua uliyoifikia unategemea
kuendelea na siasa?
Wema: Niache? Siwezi kwani itakuwa kazi yangu, kama
gari ndiyo limewaka sasa.
Ijumaa: Najua siasa ni hela hasa kipindi cha
kampeni, uliwezaje kumudu gharama zote?
Wema: Ni rahisi sana ukiwa na watu wanaokupenda,
walijitokeza watu kunichangia kwa ajili ya kuhakikisha nafanikiwa. Siwezi
kuwataja lakini nawashukuru sana.
Ijumaa: Tulipata habari kwamba baada ya kushindwa
uliangua kilio, kwa nini?
Wema: Unajua unapoenda kufanya kitu lazima una
matumaini japo kuna kushindwa lakini kushinda ndiyo lengo sasa usipofanikisha
lazima roho inauma.
Ijumaa: Ulijisikiaje ulipokuta nyomi la watu
wakikusubiri kwa ajili ya kukupokea wakati hukuwa umeshinda?
Wema: Niliamini nina watu wengi ambao wananipenda
na nilijifunza mengi kupitia ujio wao, pia walinitia moyo wa kuendelea na
siasa.
Ijumaa: Kuna madai kuwa baada ya kushindwa una
mpango wa kuhamia Ukawa, hilo unalizungumziaje?
Wema: Ninachojua watu wa Ukawa wamenitafuta na
ilikuwa tukutane jana (Jumatatu) ila tutakutana Jumatano (juzi), nikijua
wanachoniitia ndiyo nitafanya uamuzi.
Ijumaa: Baada ya kuingia kwenye mambo ya siasa
tumtegemee Wema wa aina gani?
Wema: Mtarajieni Wema wa tofauti na yule
mliyemzoea, mambo ya skendoskendo hayatakuwa na nafasi kwenye maisha yangu.
Hakuna maoni