Hii ndio sababu iliyofanya Mbunge Andrew Chenge hajafika leo kuhojiwa na Kamati ya Maadili Dar…

3X6A7798
Ni zaidi ya miezi saba imepita toka Bunge litoe mapendekezo kwamba wahusika wote wa ishu ya ESCROW wawajibishwe, kazi ikaanza kwenye Kamati ya Maadili ambapo Viongozi mbalimbali walianza kuhojiwa ikiwemo Mbunge Anna Tibaijuka, Andrew Chenge na William Ngeleja.
Kwa upande wa Andrew Chenge Kamati hiyo ilisimamisha kumhoji kwa vile alikuwa amepeleka ombi Mahakama Kuu kuzuia kuhojiwa, baadae Mahakama hiyo ikatoa amri kwamba Kamati ya Maadili inaweza kuendelea na kumhoji.


3X6A7825 
July 27 2015 ilikuwa Mbunge huyo afike kwenye Kikao cha Kamati ya Maadili Dar kwa ajili ya kuhojiwa na kuhusika kwake kwenye ishu ya ESCROW, lakini ripota wa millardayo.com kafika kwenye Ofisi za Kamati hiyo.


3X6A7800




 
Mbunge huyo hakufika na taarifa iliyotolewa ni kwamba Andrew Chenge ameomba Kamati ya Maadili ipeleke mbele tarehe ya kusikiliza shauri lake kwa vile ratiba hiyo inaingiliana na majukumu yake ambayo CCM imemkabidhi Jimboni kwake Bariadi Magharibi wakati huu wa maandalizi ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015.
 
3X6A7826

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.