Hii ni hukumu iliyotolewa leo JULAI 28 na mahakama ya Libya kwa mtoto wa Gaddafi …
Mahakama ya Libya leo imetoa hukumu kwa mtoto wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Gaddafi, aitwaye Saif al Islam na wenzake nane kufuatia uhalifu wa kivita uliohusishwa na mapinduzi ya mwaka 2011.
Wote walikuwa wameshtakiwa pamoja sasa wamehukumiwa kunyongwa pamoja
na washirika wengine wa kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani kwa
kujaribu kazima maandamano wakati wa mapinduzi hayo.
Mtoto wa Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi aliyehukumiwa kunyongwa
Kwa sasa Saif anazuiliwa na kundi moja la waasi la zamani katika mji wa Zintan ambapo wamekataa kumuachilia huru.
Hakuna maoni