Hatimaye kaka Yake Zari Amchumbia Mwanamuziki Linah Sanga....
Hatimaye staa wa Bongo Fleva ambaye ni zao la Nyumba ya
Vipaji Tanzania (THT), Esterlina Sanga ‘Linah’ amechumbiwa rasmi na yule jamaa
wake, Wiliam Bugene ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka kiukoo wa mpenzi wa mwanamuziki
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.’
Akizungumza na Amani kwenye mahojiano maalum alipotimba
katika Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF), Zanzibar hivi karibuni, Linah
alisema kuwa ana furaha maishani mwake kwa kumpata mtu mwenye mapenzi ya kweli
ambaye atafunga naye ndoa ‘soon’.
“Tayari ameshanichumbia, anajulikana kwetu na mimi
najulikana kwao. Kifuatacho ni ndoa yangu,” alisema Linah ambaye hivi karibuni
amesema ataachia wimbo mpya utakaokuwa gumzo.
Furaha ya Linah inakuja kufuatia kumpata mwanaume huyo
ambaye amekuwa akionekana naye kila kiwanja wakiwa wamegandana kimahaba ikiwa
ni miezi kadhaa tangu alipodai kuporwa bwana’ke, Nagari Kombo anayedaiwa
kakwapuliwa na Wema Sepetu.
Kabla ya Boss Mtoto na Kombo, huko nyuma Linah aliwahi
kuripotiwa kuwa kwenye uchumba ‘serious’ na msanii mwenzake, Amini Mwinyimkuu.
Hakuna maoni