Kutoka kwenye Mkutano wa CCM Dar July 29 2015>>> Dk. Magufuli, Uchaguzi 2015.. Lowassa kuhama? Wengine waliotoka?
Kulikuwa na tangazo ambalo lilienea sana
mitandaoni kuanzia July 28 2015 ikiwa na taarifa kwamba CCM watafanya
Kikao chao Makao Makuu Madogo July 29 2015 Lumumba Dar.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Dar, Juma Simba Gaddafi ndio Kiongozi pekee wa CCM aliyefika kwenye Mkutano huo ambao umefanyika Peacock Hotel Dar, na hii ni sehemu ya alichokisema.
‘CCM
inatoa shukrani kwa ushirikiano mlioutoa katika Mkutano wetu Mkuu wa
Kumtambulisha Mgombea Urais Dk. Magufuli pale Mbagala, CCM ni Chama
chenye busara tumeona tuwashukuru‘>>>
Kwenye sentensi nyingine amesema hivi >>> ‘Tume
ya Uchaguzi tunawaomba wawe makini kuongeza Mashine na Watendaji ili
watu wapate nafasi kujiandikisha na watumie fursa yao Kupiga Kura… CCM
tuna uhakika tutashinda‘>>>
‘Kingine
tunawashukuru waliojitokeza Kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na
wajitokeze kwa wingi pia kupiga kura… Tumemaliza Uchaguzi Dodoma na
kumpata Mgombea wetu Dk. Magufuli, tunajivunia kwa sababu ana rekodi
nzuri… Tuna imani CCM itaendelea kuongoza 2015 mpaka 2020, tumefanya
mengi yanayokubalika‘>>>
Hiki ndio alichokijibu kuhusu ishu ya Lowassa kuhamia CHADEMA >>> ‘Yeye
aliingia CCM kwa ridhaa yake hakuna mtu alimlazimisha, ametoka kwa
ridhaa yake na CCM itabaki kuwa CCM… Wafuasi walikuwa ndani ya CCM,
kuondoka kwake ameondoka yeye na sio wa kwanza kuondoka‘>>>
Haya ni majibu yake mengine kuhusu Lowassa kutoka CCM >>> ‘Mtu
akitoka huwezi kujibu kwa nini ametoka, nawathibitishia mtu yoyote
akitoka CCM itabaki imara… Tutashinda asubuhi kweupe… Kama Lowassa
angekuwa anaondoka na watu wengi ungewaona jana, lakini alikwenda yeye
akarudisha kadi… watu wengi wanatoka kwenye Chama na CCM bado iko imara‘ >>>> Juma Simba Gaddafi.
Hakuna maoni