Birdman kafanya interview kaongelea ukweli kuhusu ugomvi wake na Lil Wayne!!


1112
Kumekuwa na stori nyingi sana kuhusiana na ugomvi wa Lil Wayne na Birdman, tukasikia kuwa Lil Wayne anataka kuondoka Cash Money Records kwasababu Birdman hataki kumlipa hela yake.
Tukasikia ugomvi umefikishwa Mahakamani na Lil Wayne amesisitiza kuwa ataondoka na wasanii aliokuja nao, Nicki Minaj na Drake kama Birdman hatamlipa pesa anazomdai…Lil Wayne anataka dola mil. 51 (Bil 102 za Tz).
bird and angie2
Birdman na Angie Martinez wakiwa wanarekodi interview yao kwenye boti ya Birdman.
Birdman kaamua kumuita radio personality Angie Martinez nyumbani kwake Miami kufanya nae interview kuhusu ugomvi huu, Birdman alikuwa na haya ya kusema…
bird and angie4
Angie Martinez alivyowasili nyumbani kwa Birdman jijini Miami.
>>> Lil Wayne ni mwanangu, haijalishi kumetokea nini…nataka afanye maamuzi kwa faida na maslahi yake, nilikutana na Wayne akiwa hana chochote nikamlea kama mwanangu na amekuwa mwanangu, mimi na yeye tuliibadilisha gemu ya rap Marekani…<<<Birdman.
bird and angie8
Wakiwa ndani ya boti ya Birdman na kuzungumza.
>>> Nilishawahi kumpatia Lil Wayne mkataba wa zaidi ya dola milioni 100 na kutanguliza dola milioni 67 za advance na mpaka leo huo ndio mkataba wa bei juu zaidi kwenye hii industry…sasa sielewi haya maneno yanatoka wapi lakini kama nilivyosema Wayne ni mtoto wangu atakachokifanya nitamsupport.<<< Birdman
bird and angie9
Birdman C.E.O wa Cash Money Records (CMR)
>>> Sitaki aondoke, lakini mpaka sasa sijasikia kauli yoyote ya yeye kutaka kuondoka ikitoka mdomoni mwake, akinifuata na kusema baba nahisi umefika wakati wa mimi kufanya yangu nitamruhusu, awe au asiwe na mimi yule ni mwanangu na nitamsupport kwa kila kitu. <<<Birdman
bird and angie
Badaae walitoka ndani na kumalizia interview yao nje ya boti huku wakienjoy upepo mzuri wa bahari jijini Miami.
>>> “Nilianza hii biashara nikiwa na miaka 17 na cheque yangu ya kwanza ilitoka Universal Records nikiwa na miaka 19 na ilikuwa ya dola Mil.30…nimetengeneza pesa mno kwa nini nitake kumuua Lil Wayne? Nadhani wanajaribu kutuvuta kutokana na makundi ya kibiashara alafu na nyie watu wa media mnachochea”. <<< Birdman
bird and angie6
Muonekano wa boti ya Birdman kwa nje.
>>> “Lil Wayne akitaka kuondoka sawa nitamsupport, siwezi kumtema kisa kaachana na mimi, kama baba haitakuwa sawa kumfanyia hivyo mwanangu… Kuhusu Nicki Minaj na Drake,hapana wale hawataondoka na Wayne, Wayne kuondoka haimanishi na wao wataondoka”. <<<Birdman.
birdman-1
Badaae chakula kikaletwa mezani…
>>> “Sijui kilichotokea siku ile, mimi sikuepo mjini siku hiyo na nilisikia kuwa basi la Lil Wayne lilipigwa rasasi, na nataka ujue kitu… mtu yoyote akijaribu kumtishia Lil Wayne maisha basi amini mimi na huyo mtu tutakuwa na matatizo makubwa, lakini mimi kupanga kumuua ni kitu cha kijinga“. <<<Birdman. 
Kuhusu kumwagia Lil Wayne pombe, Birdman alisema kuwa yeye hawezi kumfanyia hivyo mwanae na kwanza hawezi kufanya hivyo kwa mtu yoyote.
Hapa chini ipo  exclusive interview nzima ya Birdman na Angie Martinez.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.