Birdman kasemaje kuhusu tuhuma za kumpiga risasi Lil Wayne,Stori iko hapa.


Birdman
CEO Wa Cash Money Records Birdman amesema hajahusika kabisa na njama za kumpiga risasi rapa Lil Wayne.
Mwezi wa sita kesi ilifunguliwa dhidi ya Birdman na Young Thug wakishutumiwa kuhusika na njama za kumpiga risasi rapa Lil Wayne akiwa kwenye basi lake la tour, kesi hio pia ilimtaja menja wa ziara za Young Thug ‘Jimmy Carlton Winfrey ‘ akiwa miongoni mwa watu waliohusika kupiga risasi gari la tour la Lil Wayne mwezi wa nne.
Birdman amesema hana ukaribu wowote na Winfrey ila mpaka sasa polisi wanaushahidi kuwa Birdman na Winfrey waliongea kwenye simu dakika chache baada ya tukio hilo.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.