Watoto wa mastaa wa soka waliofuata nyayo za baba zao (picha & video) zipo hapa
Huwa ni kawaida sana kwa watoto kupenda kufanya kazi
wanazofanya wazazi wao, kwa maana nyingine haishangazi kuona baba akiwa Doctor
na mtoto akaja kuwa Doctor au mzazi polisi na mtoto akaja kuwa polisi hii
inaweza isitokane na maamuzi ya mtoto wala shinikizo la mzazi kwani mazingira
anayokulia humfanya aanze kufuata nyayo za mzazi wake.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa wanasoka wengi ambao
hupenda kwenda na watoto wao uwanjani katika mechi za fainali au mechi zozote
na mara nyingi utabiriwa kuja kuwa wanasoka mfano mwaka 2012 kocha wa Arsenal
Arsene Wenger alikuwa wa kwanza kuomba
kumsajili mtoto wa Lionel Messi
ili akikua ajiunge na Academy ya Arsenal.
Nimekusogezea picha na video za watoto wa mastaa
waliofuata nyayo za baba zao.
1. Enzo Zidane
ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Ufaransa na klabu ya Real
Madrdid ya Hispania Zinedine Zidane...
Enzo amefuata nyayo za
baba yake na hivi sasa yupo katika timu ya vijana ya Real Madrid Enzo ni mjanja
na anajua kuuchezea vizuri mpira kama baba yake.

Enzo na baba yake
Zidane
2. Rivaldinho ni mtoto wa
Rivaldo staa wa soka
kutokea Brazil lakini pia amewahi kuichezea FC
Barcelona ya Hispania kwa mafanikio, Rivaldinho amefuata nyayo za baba yake kwa
kuanza kuichezea klabu iliyomlea baba ya Mogi Mirim na kwa sasa wanacheza
pamoja na baba yake katika klabu hiyo.

Rivaldo na mtoto wake
Rivaldinho
3. Tom Ince ni mtoto wa staa wa
zamani wa Uingereza Paul Ince
ambae amewahi kutamba katika vilabu vya West Ham United, Manchester United na
Liverool ila Tom
anachangamoto kubwa ya kupata mafanikio kama aliyofikia baba yake. Tom Ince kwa sasa anaichezea Derby
County.

Paul Ince na mtoto
wake Tom
4. Justin Kluivert yupo katika
Acacdemy ya Ajax Uholanzi baba yake Patrick Kluivert amewahi
kutamba katika klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi.

Justin Kluivert na
baba yake Patrick Kluivert
5. Joe van der sar ni mtoto wa
golikipa wa zamani wa Manchester United Edwin van der sar amefuata
nyayo za baba yake si kwa kucheza soka tu bali hata nafasi anayoichezea ni sawa
na baba yake. Joe yupo katika Academy ya Ajax.

Joe na baba yake
Edwin van der sar
Hakuna maoni