BASATA imemfungia Shilole mwaka mmoja, hakuna kufanya muziki
‘BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013BASATA lilikuonya na
ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza
bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA
ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini
usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako
lakini umekaidi kutoa maelezo yako‘ – BASATA
‘Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya
sanaa kwenye onyesho lako
huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30
(2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo
baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini
na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na
hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote
utakaeshirikiana nae ‘ – BASATA
Hakuna maoni