Ni kweli Tundaman kadhulumu ela ya usafiri? kasikika kwa Soudy Brown leo…#UhearD JULY28
Soudy Brown kazungumza na jamaa anayedai kudhulumiwa ela yake ya usafiri baada ya kupewa kazi ya kupelekana na kurudisha vifaa vya kushoot video ya ‘Qaswida’ ya Tundaman kutoka Changanyikeni hadi Lamada.
Amesema walikubaliana wamlipe 60,000 lakini baadaye akaanza kuzungushwa na kila akimpigia simu hapokei hadi baada ya wiki na kuahidi atamtumia lakini mpaka sasa hajamtumia.
Tundaman mwenyewe amesema alimwambia aje kuchukua lakini hakuja, na yeye hawezi kumdhulumu na yupo tayari kummalizia fedha yake iliyobaki ambayo ni 25,000.
Wasikilize hapa…
Hakuna maoni