Ne-Yo Aeleza Kwanini Alikuwa na Hamu ya Kuonana na Diamond Platnumz Alipoenda Afrika Kusini
“Baada ya watu kusikia kuwa nilikuwa nakuja kwenye MAMAs jina pekee ambalo walikuwa wakilitaja kwangu ni Diamond Platnumz,” Ne-Yo alimwambia Vanessa Mdee kwenye interview ya MTV Base.
“Nikasema ni lazima nikutane na huyu jamaa, nahitaji kumuona,” aliongeza.
Siku moja kabla ya tuzo hizo pia, Diamond alielezea jinsi Ne-Yo alivyomtafuta. “Wakati nazungumza na D’banj @salaam_sk alinifata na kuniambia @neyo anakutafuta anataka kukuona…” Ungependa kujua kilichofata??? Kaa karibu na TV, Radio yaani Kiufupi Media zako Soon utayaskia,” aliandika Diamond kwenye Instagram.
Ne-Yo na Diamond ni miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye MTV MAMA 2015.
Hakuna maoni