Breaking News | International News | Political | Business | Sports | Games | Entertainments | Global Music | East Afrika | Bongo Flavour | Bongo Movie | Udaku wa Social Media
Home/
Unlabelled
/ Maamuzi rasmi ya ACT Wazalendo kupitia kwa Zitto Kabwe kuhusu kujiunga na UKAWA
Maamuzi rasmi ya ACT Wazalendo kupitia kwa Zitto Kabwe kuhusu kujiunga na UKAWA
Headlines zimeendelea kwenye mwaka huu wa Uchaguzi 2015 ambapo UKAWAsio
jina geni kwa Watanzania, vyama mbalimbali vya upinzani vikiwemo
CHADEMA na C.U.F vilijiunga na vinataka kumtangaza mgombea mmoja
atakaewawakilisha. Zitto Kabweambaye aliondolewa kwenye chama chaCHADEMA,alijiunga na chama chaA.C.T WazalendoMarch 2015 ambapo siku kadhaa baadae chama hicho kilitaka kujiunga naUMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA)lakini imeshindikana, haya hapa chini ndio maneno ya Zitto KabweJuly 26 2015.
‘Leo
siku nzima nilikua nina kikao cha mashauriano na viongozi wa chama wa
kata zote za mkoa wa Dar es salaam ( mikutano mikuu ya majimbo 10 ya
Dar) jumla ya wajumbe 1023 walihudhuriam, tumesisitiza kuwa hatutajiunga UKAWA…ikumbukwe kuwa tuliomba utaratibu wa kujiunga UKAWA mwezi Aprili mwaka 2015 na hatujajibiwa rasmi lakini moja ya chama ndani yaUKAWAkilitangaza kuwa hawatutaki‘ – Zitto Kabwe
‘Hata juzi kwenye gazeti la Mawio waliandika kuwa tumefukuzwaUKAWA,sisi
tumeamua kuingia kwenye uchaguzi wenyewe.. tarehe 10 Agosti 2015
tutatangaza mgombea Urais tutakayemuunga mkono baada ya mkutano mkuu wa
kidemokrasia wa ACT Wazalendo. Tutanadi ‪#‎AzimioLaTabora‬ kama zana ya kuleta mapinduzi katika nchi yetu‘- Zitto Kwenye sentensi nyingine ya Facebook aliyoandika Zitto Kabwesaa kadhaa kabla ya hiyo ya juu aliandika >>> ‪#‎ACTWazalendo‬ Tutaingia
kwenye uchaguzi wenyewe. We will go it alone as a party to defend our
principles. Mkutano Mkuu wa Chama wa Kidemokrasia ( National Convention)
utafanyika tarehe 10 Agosti 2015′
Hakuna maoni