Inspector Haroun kazungumzia ugomvi wake na Luteni Kalama…
Wiki iliyopita Luteni Kalama alilalamika kuwa Inspector Haroun
anamuhujumu ..leo Inspector kafunguka kuhusu shutuma hizo na kusema
waliachana mwaka 2012/13 yeye akibaki kama msanii wa kujitegemea wakati
mwenzake akiwa kundi la Wanaume family.
Jamaa anasema baadhi ya watu walitaka
walirudishe kundi bila mafanikio kutokana na Kalama kutokuwa na msimamo
na alimchukua kwenye shoo yake lakini si za Gangwe Mob bali ni yake mwenyewe.
Kuhusu kumuaibisha mke wake anasema
hajagombana na mwanamke huyo bali alimshirikisha kwenye nyimbo yake
akimtaka wafanye video kabla ya ramadhani lakini yeye alikataa kutokana
na kutojiandaa kitu ambacho kiliwachukiza Kalama na mpenzi wake.
Hakuna maoni