Edward Lowassa ni Adui Mbaya kwa CCM Kuliko Adui Yeyote Waliyewahi Kupambana Naye
Chadema waliumizwa mda mrefu sana na Zitto kwakuwa walikuwa wanapambana na adui wasiyemjua, siku walipomjua walimtupa nje na sasa usalama wa chadema umeimarika maradufu.
Ni bora kupambana na Adui aliyejitangaza rasmi kuwa yeye ni adui kwako kuliko yule unaekula nae na kulala nae bila kujitangaza kwamba ni adui kwako.
Lowasa anaweza kuwa adui mbaya kwa ccm kuliko adui yeyote waliyewahi kupambana nae. Kwa habari njema nikuwa majemadari wa ukombozi wakiongozwa Ally Bananga diwani wa Sombetini wamevamia kwa mikutano Monduli ilipo Ngome ya Lowasa. Habari njema zilizopo ni kwamba amevuna madiwani wa ccm na huko pia.
Ccm watapata wakati mgumu sana endapo Lowasa ataendelea kuwa mwanachama wao kuliko endapo wangemfukuza. Madiwani kumi tayari wamerudisha kadi na wanachama wengine 30,kupitia mitandao ya kijamii imeoneshwa watu wakichana chana kadi za ccm.
Lowasa ataendeleza mapambano akiwa ndani ya jahazi. Hakika litazama. Huu ni mwaka wa UKAWA kuchanga karata zao vizuri.
Mh Lowasa, nakutahadharisha, epuka mpango wowote wakutaka maridhiano na ccm, kwani mpango huo ni hatari kwa uhai wako.
Mpango mkakati huu wa lowasa ni hatari kwa ccm kuliko yote iliyowahi kutokea.
Hakuna maoni