50 Cent kafikishwa Mahakamani na anadaiwa faini, ni kweli amefilisika??
Kumekuwa na stori nyingi kuhusiana na rapper 50 Cent kutoka Marekani, moja kubwa kuhusu yeye ilikuwa ni stori inayohusiana na yeye kuvijisha video ya ngono ya mwanadada Lastonia Leviston ili kumuaibisha mshindani wake kwenye muziki, Rick Ross.
Kesi ikaenda Mahakamani na hukumu inaonesha 50 Cent anatakiwa alipe faini ya dola Mil.5 sawa na Billioni 10 za Kitanzania kwa mwanadada huyo.
Headlines za 50 Cent
leo ziko tofauti, Mwanasheria wa rapper huyo ametangaza kwamba jamaa
kafilisika, Mahakamani zimepelekwa document zinazoonesha kuwa 50 Cent ana madeni yasiyopungua dola Mil.50 sawa na Bil.100 za Kitanzania.
Sheria inatoa nafasi kwa mtu kupeleka
Mahakamani documents na vielelezo vingine vinavyompa nafasi kujilinda na
kuokoa baadhi ya biashara zake wakiwa wanakabiliana na madeni makubwa.
Msemaji wa mwanasheria wa 50 Cent, Travis Carter amesema
msanii huyo amelazimika kufanya hivyo kuweka mambo yake ya kiuchumi
sawa lakini hii haimanishi rapper huyo hana uwezo wa kusimamia biashara
ama pesa zake.
Kwenye Interview moja 50 Cent alisema: “Kufanya
hivi kunanilinda mimi na maslahi yangu ya biashara nyingi
ninazojihusisha nazo, ni kawaida kwa wafanyabiashara kufanya hivi ni
sawa na kulinda mifuko yangu. Uwezo ninao sema narekebisha tu vitu
fulani kwa faida yangu na wadeni wangu”>>> 50 Cent.
Travis Carter alisema: “Maslahi
yake ya kibiashara yataendelea kama kawaida na ataendelea kujihusisha
na biashara zake nyingine na kuendelea kufanya kazi kama entertainer”.
Hakuna maoni