Je Muller atamfuata Schweinsteger Man Utd? Philip Lahm amejibu hapa..


Ripoti nchini Ujerumani zinasema kwamba Man United imeandaa ofa nzito kwa ajili ya Muller, taarifa zilizomfanya Lahm Kuongelea tetesi hizo za usajili.
“Kuondoka kwake sio uamuzi wangu, vitu vinatokea haraka sana katika soka. Siwezi kuwahakikishia kwamba Thomas Muller anaweza kuendelea kubaki nasi.” – Alisema Lahm wakati mkutano wa waandishi wa habari huko Shanghai China.

 Hata hivyo Lahm amesema kwamba hakuna namna ambayo yeye ataondoka Bayern kwa sasa. “Hilo haliwezi kutokea. Nina furaha kwamba nimeweza kuitumikia klabu hii kwa muda wote. Ni jambo la furaha kuwepo hapa kwa muda mrefu."

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.