Mbunge wa CCM Awakimbia TAKUKURU.......Ni Baada Ya Kunaswa Akigawa RUSHWA Kwa Wapambe Wake

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani
Manyara, imemhusisha Mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri (pichani
kulia), na tuhuma za kutoa hongo katika kura za maoni ndani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Takukuru inadai kuwa mbunge huyio alinusurika kukamatwa juzi usiku akiwa na wapambe wake waliokuwa wanagawa rushwa.
Kamanda wa Takukuru mkoani Manyara, Mogasa Mogasa, alisema
Chambiri akiwa na wezake watatu ambao wanashikiliwa na taasisi hiyo,
alinusurika kwa kutimua mbio usiku majira ya saa nne na kuacha kitita
chaSh. 500, 000 alizokuwa nazo katika kijiji cha Kiongozi akitaka
kuzigawa kwa baadhi ya watu wake.
Pia taarifa ya kamanda huyo ilieleza kuwa Chambiri
alifanikiwa kukimbia akiwa na viongozi kadhaa wa kijiji hicho ambao
kamanda huyo hakuta kuwataja majina, akisema kuwa wanaendelea kutafutwa
na kumtaka Chambiri ajisalimishe.
Kamanda huyo aliwataja waliyokamatwa kuwa ni Samuel John
Barani ambaye ni Katibu wa Uchumi na Fedha CCM wilaya; Thomas Cosmas
Darabe na Ally Ayubu Ramadhani, ambao walikuwa na mgombea huyo katika
harakati hizo.
Kamanda Mogasa aliongeza kuwa baada ya watuhumiwa hao
kukutwa katika eneo hilo na Chambiri kutokomea, walifanikiwa pia
kukamata makaratasi yenye majina ya watu waliokuwa wameandaliwa kwa
ajili ya mgawo huo.
Hata hivyo, alisema wanaendelea na mahojiano watuhumiwa hao
na kwamba baada ya taratibu kukamilika watafikishwa mahakamani na
kuongeza kuwa wanalishikilia gari la mbunge huyo.
Chambiri alipoulizwa, alikana kuhusika na kudai kuwa ni mbinu zinazotumiwa na baadhi ya watu wasiyomtakia mema.
Aidha, alidai kuwa yeye kama mgombea na mtetezi wa jimbo
hilo, amekuwa akipata taarifa mara kwa mara za kupangiwa njama kama hizo
ili kudhoofisha juhuddi zake za kurejea madarakani.
“Hivi walishindwaje kunikamata wakati wanadai walitukuta
tukiwa ndani kama siyo uzushi, mimi nafahamu kuna watu wamewekwa
kunichunga hata kama naenda nyumbani kisa tu mimi nisichanguliwe, na
hiyo ni baada ya kuona watu wameonyesha upendo kwangu,” alisema Chambiri
Hakuna maoni