Shetta hasafiri tena na Basi? Mengine yapi yamebadilika kwake? Ni haya hapa…
Ameanza kwa kusema>> ‘Kwa
mtu anayemtaka Shetta kwa sasa inabidi akubaliane na timu yangu ya watu
10 nina mpiga picha, nina security, Manager na Dancers na nina mtu wa
kuimba naye jukwaani (back vocal)’
Swali lingine ambalo ripota wa millardayo.com alitaka kufahamu ni kuhusu namna ya kusafiri kwa hiyo timu yake ambapo Shetta amesema>> ‘kwa sasa sisafiri tena na basi na kwa zile sehemu ambazo hakuna ndege mara nyingi huwa nauliza namna ya kupata usafiri binafsi‘.
Mengine amesema hata bei ya show zake kwa sasa zimepanda >>’ Watu wamemzoea Shetta wa Milion 3 au 4 sasa hivi nachaji kuanzia dolar 5,000 (zaidi ya Milion 10 za Kitanzania kwa sasa). >>>> Shetta.
Hakuna maoni