Steve Nyerere Awaumbua Mastaa Wasio ipigia Kampeni CCM
Steve Nyerere na Wema Sepetu |
STAA
wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amewachana wasanii
kwa kuwaita wanafiki kutokana na kuukacha uzinduzi wa kampeni za Chama
cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Uwanja wa Jangwani wiki
iliyopita.
Akizungumza
na mwandishi wetu juzikati, Steve alisema ameshangazwa kuona baadhi ya
wasanii kuikacha CCM na kuupigia debe Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) ambao unaundwa na vyama vinne vya Chadema, Cuf, NCCR na NLD
wakati Serikali ya CCM imewafanyia mambo makubwa.
“Hawa
wasanii ni wanafiki na ndiyo maana wakati mwingine unatakiwa kuwaambia
ukweli tu. Serikali ya CCM imetufanyia mambo mengi kwenye sanaa na kwa
kutambua hilo ndiyo maana juzi tulimuaga kwa kishindo rais Jakaya
Kikwete lakini baadhi ya wasanii tuliokuwa nao katika hafla hiyo nao
wanaiponda CCM na kushabikia Ukawa,” alisema Steve bila kuwataja majina.
Miongoni
mwa wasanii ambao wamejipambanua moja kwa moja kuwa ni Ukawa ni pamoja
na Aunt Ezekiel, Chuchu Hans, Jacqueline Wolper, Shamsa Ford, Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego, Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine kibao.
Hakuna maoni