Mwaka huu ni headlines za Uchaguzi 2015 tumeona baadhi ya wasanii
wameonesha kutoa support kwenye kipindi hiki kwa wagombea Urais wawili
ambao ni John Pombe Magufuli atakaegombea CCM na Edward Lowassa kupitia
CHADEMA.
Miongoni mwa wasanii waliojitokeza na kutangaza rasmi kumsupport mgombea
Urais kupitia CCM, Dkt.John Pombe Magufuli, kuna Wema Sepetu, Batuli,
Snura, Linex, Steve Nyerere, Diamond Platnumz, Shetta, Barnaba,Bushoke,
Kysher, Wastara na wengineo huku mwigizaji Aunty Ezekiel na Jackline
Wolper wanamsupport Edward Lowassa na sasa ni zamu ya Nay wa Mitego.
Nay wa Mitego anamsupport Edward Lowassa kayaandika haya….>>>>
Huwezi
zuia Mvua ikiamua kunyesha inanyesha tu! Tuna Imani na Lowassa. Ccm
wote bado wana Imani na Lowassa hata Kura za Urais ni kwa
Lowassa.Nilikua sipost chochote coz Nilikua nataka nisikie CCM labda
wana jipya juu ya sera yao mwaka huu coz upinzani umekua mkali,
wangenishawishi kidogo. Dooh ndo wameongeza uozo mara dufu.Watanzania
wameamka si kwa uongo ule wa jana ���� Milioni Hamsini kila Kijiji.
Tanzania ina vijiji vingapi? Piga Hesabu ya haraka kadilia, si chini ya
bilioni 600 na zaidi.Watanzania sio mazoba kiasi hicho
tumeshtuaa…Hamjajipanga mwaka huu mmetukosa..#Mabadiliko2015
Hakuna maoni