Pichaz za Balotelli akiwasili AC Milan kufanya vipimo vya afya
Mshambuliaji mtukutu ambaye amewahi kuvichezea vilabu kadhaa Mario Balotelli ameondoka Liverpool na kurejea katika klabu yake ya zamani ya AC Milan, Balotelli anarudi AC Milan ikiwa ni msimu mmoja umepita toka ajiunge na Liverpool akitokea AC Milan ya Italia kwa dau la pound milioni 16.
akiwasili kwa kufanya vipimo vya afya Milan
Balotelli anarudi Italia katika klabu ya AC Milan kwa mkopo wa muda mrefu na tayari ameshafanyiwa vipimo vya afya na yupo tayari kukitumikia kikosi hicho.
Mshambuliaji huyo wa kiitaliano mwenye asili ya Ghana amerejea AC Milan akiwa na rekodi ya kucheza mechi 16 akiwa na Liverpool na kuifungia goli moja pekee.
” Nipo
fiti nasubiri kufanya mazoezi na timu nina hamasa kubwa ninachotaka ni
kufanya kazi na sio kuongea, nilifikiri nitarudi Milan siku moja? ndio
siku zote Milan ipo katika moyo wangu na nilikuwa na matumaini kuwa
nitarudi siku moja”>>> Balotelli
Baada ya kumaliza kufanyiwa vipimo vya afya
Rekodi ya Balotelli katika vilabu alivyochezea
Hakuna maoni