Usitegemee kumuona Ivo Mapunda Simba tena! yote mapya yako hapa (+Audio)

Golkipa mkongwe aliyewahi kucheza katika klabu za Yanga na Simba Ivo Mapunda August 18 2015 amezungumzia kilichotokea kati yake na Simba mpaka kutopata nafasi ya kuongezewa mkataba kuichezea club hiyo…….. ni kupitia hii Exclusive Interview na  millardayo.com
IVO RIP DAD
Mwishoni mwa wiki iliyopita Rais wa Simba Evance Aveva alisema Ivo aliitiwa mkataba mpya na klabu ya Simba lakini hakuokea kwenye kuweka saini, ni kama alikua anakwepa hivi….  ikiashiria kwamba kama angekwenda kusaini mkataba mpya siku yoyote kabla ya August 17 kabla hazijaanza kuenea stori kwamba Simba imemtema.
Ivo anafafanua hapa pia kuhusu zile milioni 10 ambazo imesambaa kwamba anadaiwa na Club hiyo ambazo alizichuku kama mkopo.
IVO
Ivo Mapunda ameanza kwa kusema >>> “Ni maneno unajua suala la pesa ni suala la siri kati yangu na klabu ila haya maneno ya kuwa nimepokea milioni 8 ni maneno tu ila ni kweli mimi nimepokea pesa kutoka kwa viongozi wa klabu ya Simba ila hizi fununu nyingine zinakuwa  sio za kweli’
Kuhusu Mkataba kusitishwa na Simba: Ivo amesema >>> ‘Nadhani kilichokua kinakwamisha labda ni mawasiliano kati yangu na aliyepewa jukumu la kunitafuta ili nisaini mkataba mpya, huenda hakufanya kazi yake kwa usahihi…. mimi nilikua mgonjwa nikaondoka kambini ghafla Tanga nikarudi Dar kutibiwa, alipeleka taarifa kwamba nimegoma kusaini fomu nimempiga chenga hivyo Mkataba ukasitishwa, mpira una mambo mengi‘
‘Nimekwenda juzi ofisini, Ijumaa nikaenda tena na Jumatatu jana wakasema watanipa majibu….. majibu waliyonipa ni kwamba hawawezi kuendelea na mkataba na mimi….. inaonyesha kabisa kwamba huenda hawakuwa na nia na mimi manake bado muda upo ili kufunga dirisha la usajili“>>> Ivo Mapunda
Unaweza kumsikiliza Ivo kwa urefu kwenye hii sauti yake hapa chini.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.