Good news… Navy Kenzo Feat. Vanessa Mdee imegusa hapa kwenye Countdown ya Radio Nigeria…
Siku zote huwa nafurahishwa sana pale ninapoona watu wangu kutoka Tanzania
wanazidi kufanya vizuri kimuziki, sio siri wasanii wetu wanafanya sana
kazi na kwa bidii, kazi ambazo zinapata mapokezi mazuri kwenye countdown
mbalimbali za radio Africa.
Good news kwako mtu wangu wa nguvu, nimepita kwenye mtandao wa Twitter na nimekutana na post ya @The Beat 99.9 FM ya Lagos Nigeria na kwenye #AfricanTop10 countdown yao wimbo kutoka Tanzania ‘Game’ wa watu wetu Navy Kenzo waliomshirikisha Vanessa Mdee umeshika nafasi ya #1 wiki hii.
Hii ni good news sana na kusema kweli inafurahisha sana, Watanzania wanazidi kupenya kwenye soko la muziki Nigeria na sehemu mbalimbali Africa, ilianza ya Vanessa Mdee ‘Nobody but me’ sasa ni zamu ya Navy Kenzo kuipeperusha code ya #255.
Hakuna maoni