Aliyewahi Kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha Ambaye Kwa Sasa ni Mwanachama wa CHADEMA Akamatwa na Jeshi la Polisi

Tukio la kukamatwa Masha limefuatia kukamatwa kwa wanachama 18 waliokuwa kwenye harakati za kawaida za uenezi wa chama chao katika kampeni ya kawaida ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ambayo haizuiwi na sheria yoyote ile nchini.
Baada ya kukamatwa vijana hao na kufikishwa kituo cha Ostarbay, Mh Masha aliamua kwenda kufuatilia sababu za kukamatwa kwa wanaukombozi hao, ajabu alipofika tu nae akatiwa mbaroni.
Hakuna maoni