Siasa za mwaka huu ni kali, tena sana. Utamu na ukali wake umenogeshwa
na mambo matatu hasa moja ni jambo ambalo watanzania walikua wakisema
sana kuwa vyama vya upinzani vikiungana ndipo vitaweza kuitoa CCM ikuli,
hilo limetokea mwaka huu. Pili ni ile hali ambayo haikuzoeleka ya wana
CCM wakubwa kama Lowassa, Sumaye na wengineo kuhama CCM na kuenda
upinzani, hilo limetokea na kunogesha siasa za mwaka huu. Tatu ni jinsi
wagombea wa urais toka CCM na yule wa ukawa walivyo na nguvu katika
Jamii, woote wanakubalika na ni vigumu kusema nani ni zaidi ya mwingine,
hapo ndipo utamu unakolea zaidi na zaidi.
Najiuliza tu, je, ukawa wakishindwa kuitoa ccm madarakani mwaka huu,nani
au chama gani kitakuja kufanikiwa? Au hilo litamaanisha hakuna upinzani
mioyoni mwa watanzania na hivyo upinzani utaparaganyika?
Hakuna maoni