Picha za kwanza za Tudd Thomas katoka Hospital, ni baada ya kupigwa na Wezi.


2mgfl

Ijumaa usiku wa July 31 ni siku ambayo Producer wa bongofleva wa hits kama mdogomdogo ya Diamond Platnumz, Tudd Thomas alivamiwa na wezi na kumshambulia kisha kumuibia vitu alivyokua navyo usiku huo wakati akitokea Mliman City Dar es salaam.
1mgfl
Nimepata ujumbe kutoka kwa Mdogo wake Tudd Thomas ambaye anaitwa Ben kanifahamisha kuwa jioni ya August 14 Tudd Thomas aliruhusiwa kurudi nyumbani, Tudd ameruhisiwa baada ya kukaa hospitali kwa takribani wiki 2 kuanzia Hospitali ya Muhimbili mpaka baadae alipohamishiwa kwenda hospitali binafsi.
Majereha yake makubwa yalikua kwenye mikono ambako Daktari aliyemtibu anasema kulikua na asilimia kubwa mikono yake isiweze kufanya kazi tena kutokana na kupigwa na mapanga ya Wezi.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.