Picha na video za Messi alivyokasirika akampiga kichwa huyu jamaa wa AS Roma ndani ya Uwanja…
Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi alishindwa kuzuia hasira zake baada ya kupigwa kikumbo na Mapou Yanga-Mbiwa wa klabu ya AS Roma ya Italia,
tukio hilo lilitokea katika mchezo wa kirafiki ambapo timu zote mbili
zilikuwa zinautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mwanzo wa
msimu.
Messi akiwa na hasira alimfuata Yanga-Mbiwa na kumpiga kichwa na mwamuzi hakuwaacha, aliwapa kadi za njano wote wawili, mchezo ulimalizika kwa FC Barcelona kushinda kwa jumla ya goli 3-0 magoli ambayo yaliwekwa wavuni na wachezaji Neymer dakika ya 26, Messi dakika ya 41 na Rakitic akahitimisha goli la mwisho dakika ya 66 ya mchezo.
Cheki video ya tukio lenyewe ilivyokuwa.
Hakuna maoni