Nuh Mziwanda: Wengi Walimshauri Shilole Aniache
Nuh amesema watu walimpatia ushauri huo Shilole, baada ya hivi karibuni kusambazwa sauti yake katika mitandao ya jamii akisikika kumtaka kimapenzi msanii wa Bongo Movie Wema Sepetu, mazungumzo yao yalikuwa yamerekodiwa kwa njia ya simu na kusambazwa na mtu asiyejulikana.
Nuh Mziwanda amesema baada ya sauti hiyo kusambazwa watu wengi walikuwa wakimpigia simu Shilole na kumshauri aachane naye lakini anamshukuru Mungu, Shilole hajaweza kuwasikiliza na wanaendelea poa na maisha yao kama wapenzi na kudai Mungu ana kusudio lake kufanya waendelee kuwa pamoja.
"Wengi mlishauri aachane na mimi, ila Mungu ana kusudio lake kufanya tuendelee kuwa pamoja na nampenda sana Shishi wangu na sifikirii kumuacha," alisema Nuh Mziwanda.
Baada ya kauli hiyo ya Nuh Mziwanda mashabiki wake katika mitandao ya jamii walimbadilikia na kusema kuwa anapenda sana mteremko na kutafutiwa ndiyo maana anahangaika na watu ambao wamemzidi umri, huku wengine wakionyesha kutopenda mambo yake ya ndani anavyoanika katika mitandao ya kijamii hususani kuhusu mapenzi yake na mchumba wake.

Hakuna maoni