Professor Jay kapita kura za maoni Ubunge huu hapa
Stori ninayotaka kukusogezea ni hii
kutoka kwa mkongwe wa Hip Hop Joseph Haule aka Professor Jay ambaye wiki
zilizopita alishinda kura za maoni kupitia chama cha Demokrasia na
Maendeleo katika Jimbo la mikumi Morogoro.
Sasa leo Agosti 7, 2015 amekutana na
ripota wa TZA na kupiga naye stori kuhusiana na mchakato wa kura za
maoni jinsi ulivyofanyika.
‘Namshukuru
Mungu kura za maoni zimeenda vizuri, niwapongezi tu watu wa CHADEMA kwa
kutimiza demokrasia na tuliweza kupga kura na nimeweza kuibuka mshindi
baada ya kupata kura 240 n Mpinzani wangu DR. Salvatory Makweta 18,
Brendan Maro 15, Mkumbata 5 lakini niseme kwamba ule ushindi sio
kuonesha Jay ameshinda au anajua sana nawashukuru sana watia nia wote
walikuwa wana nguvu na wote walikuwa na uwezo’- Professor Jay
‘Baada ya
kushinda kura za maoni nimepita kuwashukuru wananchi kwa kunichagua
wajua wa kamati kuu zile za kata lakini pia nimewaomba watia nia
wenzangu wahusike moja kwa moja kwenye hizi kampeni na kwa moyo
wamekubali na ndio wataendeza kampeni zangu kwasababu naamini kupitia
elimu zao kila kitu kitaenda sawa’ – Professor Jay
.
Hakuna maoni