Baba Levo na safari ya Udiwani wake Kigoma imefikia hapa.. Baba Levo
2015 Historia inaandikwa Tanzania kwenye
Siasa, Vijana wengi wamehimizwa kuingia kwenye Kugombea nafasi
mbalimbali za Uongozi na wameitumia vizuri nafasi hiyo… Wasanii wako
kwenye headlines, wapo waliofanikiwa kupenya kwenye hatua za mchujo wa
kwanza na wapo ambao Kura hazikutimia pia.
Staa wa Bongo Fleva na comedy pia, Baba Levo aliaga Dar es Salaam kwamba anahamishia nguvu Kigoma kwa ajili ya Kugombea Udiwani kupitia Chama cha ACT- Wazalendo ambacho kinaongozwa na Zitto Kabwe.
Baba Levo
amesema waliogombea kupitishwa nafasi hiyo walikuwa sita lakini wanne
walijitoa na walibaki wagombea wawili tu kwenye hatua ya mwisho ambao ni
Baba Levo na Mzee Manyoni… Kwenye jumla ya Kura 67, Mzee Manyoni alipata Kura 20 na Baba Levo
alipata Kura 47, Ushindi uko kwake na anasubiri Uchaguzi wa October
2015 ili kama akipita hapo basi awe tayari kafikia kilele cha safari
yake kwenye Udiwani.
Hii ni post ambayo kaiweka kwenye ukurasa wake @Instagram, yuko na watu wake mtaani wanashangilia hivi..
Hakuna maoni