Ni stori ambayo imechukua headline kwa mwenyekiti wa chama cha
Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowejana Aug 10 2015 baada ya
kumaliza harakati za kumsindikiza Edward Lowassa kuchukua fomu ya Urais
kwenye tume ya taifa ya uchaguzi, alipelekwa hospitali baada ya kupata
kizunguzungu kikubwa.
Sasa leo Agosti 11, 2015 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae
ni mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter ameandika ujumbe wa pole kwa
mwenyekiti huyo baada ya kuumwa ghafla.
‘Afya ni Muhimu kuliko jengine lolote. Pole sana Mwenyekiti kwa
kuumwa ghafla. Wagombea na wapiga debe tupime afya’ – Ridhiwani Kikwete.
Hakuna maoni