Maamuzi haya Julio kuhusu Juma Kaseja na Jerson Tegete
Juma Kaseja
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Jerson Tegete na golikipa Juma Kaseja ambao kwa sasa hawana timu za kuchezea baada ya Tegete mkataba wake na Yanga kumalizika hivyo kubakia kama mchezaji huru asiye na timu na kwa upande wa Juma Kaseja yeye alikuwa na mkataba na Yanga kabla ya kuingia katika mgogoro na klabu hiyo kufikia hadi hatua ya kupelekana mahakamani.
Jerson Tegete
August 4 kocha wa klabu iliyopanda daraja msimu huu kutokea Shinyanga Mwadui FC Jamhuri Kiwelu Julio ametangaza kuwepo na uwezekano wa kuwaongeza katika kikosi chake licha ya kuwa ameshasajili wachezaji 26 hadi sasa. Julio
anaamini wachezaji hao wanaviwango na wanaweza kupata nafasi ya kucheza
na kuonyesha uwezo wao kwani wao wametanguliza kucheza zaidi kuliko
pesa.
“Mimi
bwana nimeshamaliza usajili, nimesajili wachezaji 26 wachezaji pekee
ambao naweza kuwasajili kama mipango yangu itaenda vizuri ni Jerson
Tegete pamoja na Juma Kaseja ni wachezaji ambao nimefanyanao mazungumzo
na hawakutanguliza kipato kwa hiyo mimi wamenivutia”>>> Julio Kiwelu
Hakuna maoni