Louis van Gaal akubali yaishe, kafanya maamuzi magumu
Van Gaal ambae alitangaza wiki mbili nyuma maamuzi kuhusu golikipa David de Gea kuwa hawezi kumuuza kwenda Real Madrid ya Hispania kwani bado ana mchango Man United lakini sasa Van Gaal ameonyesha dalili za kukata tamaa na maamuzi yake kwani ameagiza bodi imuuze De Gea.
Kocha huyo ameiomba bodi ya uongozi wa klabu ya Manchester United ifanye maamuzi hayo kabla ya kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu Uingereza kwani haoni kama De Gea anafurahia uwepo wake Man United.
Add caption |
“Kuna hali ambayo sio nzuri kwetu na David de Gea labda anataka kuondoka, anataka kuondoka”>>> Van Gaal
Awali zilitoka taarifa za Van Gaal kutaka kumuacha kikosini De Gea hadi amalize mkataba wake ila hali aliyoiona Van Gaal kwenye mchezo dhidi PSG ambapo Man United walipoteza mechi hiyo kwa jumla ya goli 2-0 inamlazimu akubali kumuachia.
Hakuna maoni