Super Model Naomi Campbell matatani ahukumiwa kifungo cha miezi 6 jela!!
Naomi Campbell na mpenzi wake bilionea Vladimir Dooronin
Super Model Naomi Campbell
anaziandika headlines jumamosi hii baada ya taarifa kusambaa kuwa model
huyu yupo matatani kwenda jela kufuatia tukio la ushambuliaji wa mwili
alilolifanya dhidi ya mpiga picha Gaetano Di Giovanni mwaka 2009.
Naomi Campbell alimpiga mpiga picha Gaetano Di Giovanni na pochi yake na kumparua na kucha machoni baada ya mpiga picha huyo kumpiga picha akiwa kwenye kisiwa cha Lipar Italy na mpenzi wake wa Kirussi billionea Vladimir Dooronin mwaka 2009.
Na kufikia jana Mahakama ya Sicilian Court iliyopo Italy
ilifikia maamuzi na kuona kuwa Model huyo amefanya kosa la ushambuliaji
na kumpatia kifungo cha miezi sita jela. Japo inaonekana kuwa ni
kifungo cha kwenda kukaa jela ishu ya Naomi iko tofauti kidogo.
Hili ni tukio la kwanza ambalo limempeleka Naomi Campbell Mahakamani na amehukumiwa kifungo cha A Suspended Prison Sentence
ambacho kinampa mhalifu wa mara ya kwanza wa makosa madogo muda wa
kutimiza vigezo na wajibu flani bila kuvunja Sheria na akitimiza vigezo
na wajibu huo bila kuvunja Sheria basi Mahakama inamfutia mashitaka.
Licha ya tukio hili kutokea mwaka 2009 Mahakama ya Italy
ilisema kuwa walilazimika kuisikiliza kesi hiyo kutokana na ukubwa wa
jina la model huyo akiwa ni kioo cha jamii anayetazamwa na kupendwa na
wengi duniani ili kuondoka upendeleo unaotokana na sababu za umaarufu
wake.
Hakuna maoni