Naibu Waziri wa Kazi na Ajira , Dk. Makongoro Mahanga Atangaza Kuihama CCM......Asema Atahamia CHADEMA
Dr. Mahanga ambaye ni Mbunge anayemaliza muda wake kwenye Jimbo la Segerea kwa tiketi ya CCM ametangaZA azma hiyo leo mchana baada ya rufaa yake ya kupinga ushindi wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kipawa mama Kivela kutupiliwa mbali na Ofisi ya CCM mkoa wa Ilala.
Duru za Kisiasa zinasema kilichomponza Dr. Mahanga ni kitendo chake cha yeye kuhusika katika mpango wa kumnadi Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwenye nafasi ya Urais wa CCM, ambaye kwa sasa ametangaza kugombea urais kupitia Chadema.
Hakuna maoni