Bendera ya Marekani ilivyoshuhudiwa inapepea Cuba kwa mara ya kwanza baada ya miaka 54 kupita…
Ni August 14 2015 inaandikwa Historia
nyingine kubwa Duniani, Marekani na Cuba ni nchi ambazo hazikuwa kwenye
uhusiano mzuri kwa muda mrefu, imeshuhudiwa kwa mara ya kwanza toka
mwaka 1961 bendera ya Marekani imepandishwa kwenye Ubalozi wa Marekani
Cuba kumaanisha kwamba sasa hivi kila kitu kinaelekea kuwa sawa kati ya
nchi hizo mbili.
John Kerry
anakuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Marekani kutembelea Cuba ndani ya
kipindi cha miaka 70, yeye pamoja na baadhi ya Wanajeshi wastaafu wa
Marekani wameshuhudia tukio hili la kihistoria kwenye Ubalozi wa nchi
hiyo ulioko Jiji la Havanna, Cuba.
Katibu Mkuu wa Marekani, John Kerry akiwa na mmoja ya Wanajeshi Wastaafu walioshusha bendera ya Marekani mwaka 1961 Cuba.
Historia hii inaandikwa ikiwa ni miezi
nane toka Marekani na Cuba wamekubaliana kumaliza tofauti zao
Kidiplomasia, Cuba wao walipandisha Bendera yao kwenye Ubalozi wao
ulioko Washington Marekani July 20 2015.
“Tuko
kwenye majadiliano na Cuba kwamba waweke mfumo mzuri wa Utawala wa
Kidemokrasia ambapo watu watakuwa na uhuru zaidi kuchagua Viongozi wao“– John Kerry.
Mwezi December 2014 Rais Barack Obama wa Marekani na Rais Raul Castro
wa Cuba walikubaliana kurudisha uhusiano mzuri pamoja na kufungua
Balozi za nchi zao ili kuurudisha ukaribu wa uhusiano wa nchi zao ambao
haukuwa mzuri kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Hakuna maoni