Kama vile amesahu ahadi za Ukawa kutoa elimu bure kuanzia Darasa la
kwanza hadi chuo kikuu. Jana Msigwa alipinga vikali swala la elimu bure
huku akipata kigugumizi kujibu kwa ufasaha Maswali ya Muandishi wa ITV.
Kwa hili kweli kabisa Mimi nimekushusha kabisa kwasababu Muitikio wa
elimu bure ni mkubwa sana na kila mtu anafaidi keki ya Taifa kupitia
hili la elimu bure na bila shaka ni jambo bora kabisa kumpa mtoto wa
kitanzania elimu.
Pili ni kupinga swala ya Kubana matumizi hasa kutotumia hela kwenye
sherehe na kuzielekeza kwenye Maendeleo ni jambo jema kabisa kila mtu
analisapoti kasoro wewe tu Mtumishi. Magufuli anania ya dhati kuua Siasa
za kuropoka ropoka . Zije siasa za watu wabunifu kama Professa J maneno
machache vitendo vingi.
By Pascal Ndege
Hakuna maoni