Baada ya kufungiwa na Serikali Jana, Snura kayaongea haya kwa waandishi wa habari leo
May 04 2016 Wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo leo May 04 2016 ilitangaza kuufungia wimbo wa Snura ‘chura’ kuchezwa kwenye MEDIA mpaka hapo Snura atakapoifanyia marekebisho video ya wimbo huo na kutoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii.
Leo May 05
2016 Snura Mushi amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia ishu
ya kufungiwa wimbo wake wa ‘chura’, mbele ya waandishi wa Habari Snura
amewaomba radhi wananchi kwa kutoa nyimbo ya ‘chura’ ambayo
imesitishwa na wizara ya Habari utamaduni Sanaa na michezo baada ya
kuona nyimbo hiyo ina udhalilishaji na haipo kimaadili ya kitanzania.
Snura
Mushi ameahidi kutotoa tena video yenye maudhui kama yale na tayari
ameruhusiwa kufanya show katika majukwaa mbalimbali baada ya kujisajili
baraza la Sanaa la Taifa na kupewa cheti.
Hakuna maoni