Kumbe Ryan Giggs ni player,mke wake achoshwa na hii tabia na kuchukua hatua kali.
Tuhuma hizi zimeibuka tena baada ya ukaribu wa kimapenzi wa Giggs na mfanya kazi wake wa kike kwenye mgahawa wake uliopo mjini Manchester.
Giggs na mke wake walifunga ndoa September 2007,katikati hapa Gigs alihusishwa kumsaliti mke wake na wanawake kama model Imogen Thomas na mke wa mdogo wake Natasha Lever ila alitumia nguvu na pesa kuzuia stori hizi kusamba kitu ambacho kilishindikana kwa asilimia 100.
Taarifa mpya zinasema mke wa Giggs anataka talaka yake sasa.
Hakuna maoni