Rais Samia Suluhu: Wakuu wa Mikoa hakikisheni mnawapanga upya Wamachinga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mikoa nchini kuwapanga upya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga bila kutumia nguvu ili wafanye biashara zao kwa kufuata taratibu zilizowekewa .
Amesema hayo leo katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua jana tarehe 12 Septemba katika viwanja vya Ikulu jijini Dodoma.
“Serikali ilitoa fursa kubwa kwa machinga kufanya biashara za kujipatia kipato kwa uhuru lakini msitumie fursa hiyo vibaya na kufanya biashara kiholela ambapo baadhi yao hupanga bidhaa nje ya maduka na kuwazuia wenye maduka kufanya biashara , kitend
Hakuna maoni