MAELEKEZO YA CCM KWA WAKALA WA CHAKULA KUHAKIKISHA WALIORODHESHWA MANISPAA SONGA MAHINDI YANANUNULIWA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka Wakala wa Chakula (NFRA) kuweka utaratibu mzuri ili kumaliza sintofahamu iliyopo kuhusu ununuzi wa mahindi katika Manispaa ya Songea mkoani wa kuhakikisha wananchi wote waliokwisha kuorodheshwa mahindi yao yananunuliwa.
Pamoja na kuongezwa kwa kituo kimoja cha ununuzi wa mahindi ili kuepuka msongamano katika kituo kinachotumika sasa na kuwaondolea wananchi usumbufu.
Hayo yalielezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka alipotembelea wakala huo na kujionea shughuli za ununuzi zinavyoendelea pamoja na kusikiliza wakulima waliokuwa na mahindi nje ya geti la wakala huo.
"Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekwishatoa Sh.bilioni 7.5 kwa ajili ya ununuzi wa tani 15000 katika hatua za awali kwa NFRA hapa Songea Mjini na fedha hizo tayari zipo kwenye akaunti zao.
"Chama kinaitaka NFRA kutoa kipaumbele kwa wananchi wote waliokwisha kuorodheshwa na kuongeza kituo kingine cha ununuzi wa mahindi ili kuepuka huu msongamano na kuwaondolea wananchi wa pembezoni usumbufu,"amesema Shaka
Amewataka wananchi kuondoa wasiwasi kwani Serikali imepanga mgao wa tani 35000 katika msimu huu kwa mkoa wa Ruvuma. Bado serikali inaendelea kutafuta masoko zaidi nje ya Nchi ili kuhakikisha mahindi yote yanapata soko.
Aidha aliwaomba wananchi kuwa wakati ununuzi ukiendelea mahindi zaidi yasishushwe hadi yaliyopo yatakaponunuliwa yote ili kuepuka hasara.Pia amempongeza Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mheshimiwa Dkt.Damas Ndumbaro kwa kuwa mtetezi wa kweli wa wananchi anaowawakilisha.
Shaka amewapongeza NFRA kwa kujiongeza na kutafuta ghala la ziada litakalotumika kuhifadhi mahindi tani elfu kumi na tano zitakazonunuliwa sasa.
Hakuna maoni