ALBAM YA WANANGU 99 YA RAPCHA YAACHIWA RASMI BOOMPLAY
Na Khadija Seif, Michuzi Tv
MSANII wa hip hop wa kibao cha Lisa Cosmas Paul maarufu kama Rapcha aachia albam yake ya kwanza aliyoipa jina la "wangu 99".
Akizungumza na Michuzi Tv Mara baada ya kuiachia albam hiyo Rapcha ameeleza kwa namna Mashabiki walivoupokea wimbo wa "Lisa" na kwa kipindi cha Miezi mitatu tu na kufanya vizuri na kushika chati za juu za Muziki wa Bongofleva.
" Kwa mara ya kwanza wimbo wangu wa "Lisa" umeweza kufikisha watazamaji milioni 1.5 kwenye
mtandao wa YouTube.
Aidha, Rapcha amempongeza Mtayarishaji wa ngoma kutoka Bongo records, P funky na kuchukua jukumu la kutayarisha na kusimamia albam hiyo na nyimbo zote zimefanyika chini ya bongo records.
Hata hivyo Rapcha amefafanua ujio wa Muendelezo wa wimbo wake wa "Lisa part two na kuwataka Mashabiki kusubiri ujio huo wa kisa chenye ukweli na chenye Mafunzo ndani yake.
Albam ya Wanangu 99 inabeba jumla ya nyimbo 10 ikiwemo Majani, Go Rapcha,unajua vibex remix,Nitakucheki,Kama unae,Tunajimwaga na zingine nyingi akiwashirikisha wasanii wanne akiwemo Femi one,King Kaka,Mapanch na Kid Golden.
Kwa upande wake Meneja uhusiano wa Kampuni ya Boomplay Harrison Lwanga Kazi yetu kubwa ni kutoa Ushirikiano wa wimbo za wasanii mbalimbali.
"Tutahakikisha tunatoa nafasi kwa Mashabiki zake kusikiliza albam hiyo kupitia Boomplay na itadumu kwa wiki 2.
Msanii wa hip hop kutoka Kiwanda cha Muziki wa Bongofleva akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa Kuachia rasmi albam yake mpya "Wanangu 99" iliyobeba takribani nyimbo 10 chini ya usimamizi wa Mtayarishaji wa ngoma p funk kutoka Bongo records.
Hakuna maoni