Kanisa Pentekoste Kusheherekea Miaka 75 Ya Kanisa Hilo Tanzania.
Kanisa la Elim Pentekoste Tanzania lenye makao makuu jijini Dodoma, linatarajia kusheherekea Jubilei ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwake yatakayofanyika siku ya jumapili uwanja wa Kwaraa mjini Babati mkoa wa Manyara.
Akizungumza na waandishi wa habari kanisani hapo mkurugenzi wa idara ya Habari na mawasiliano wa Kanisa la Elim Pentekoste nchini Askofu Zephania Bahhe, amesema maazimisho hayo yatasindikzwa na ujumbe wa neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Mithali 25-25 inayosema “Habari njema inayotoka nchi ya mbali ni kama maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu”.
Amesema Katika maazimisho hayo watazindua mkakati wao maalum wa kutimiza malengo ya kanisa hilo.
Amewakaribisha wananchi wote katika ibada hiyo itakayoanza saa mbili asubuhi hadi saa saba mchana siku ya jumapili Septemba 26,2021.
Amesema kanisa hilo mbali na kuhudumia jamii kiroho, limefanya mambo mengi katika Nyanja za Elimu na afya. Historia ya kanisa hilo ni uingereza ambapo Wamisionari walitoka nchini humo kuja Tanzania na kuanza kwa kanisa hilo mwaka 1946.
Hakuna maoni