Ubashiri wa Peter Schmeichel asema, Man United wanaweza kubeba UEFA mwaka huu

United ambayo imesogea mpaka nafasi ya nne kwenye EPL baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika uwanja wa Old Trafford magoli ya Cristiano Ronaldo dakika 51 na lile la Bruno Fernandez dakika ya 90.

“Wanaweza wakatwaa Ubingwa wa UEFA msimu huu, wanapambana kupata matokeo kwenye ligi lakini naamini wanaweza kufanya chochote kwenye ligi ya mabingwa kwa kuwa ni kitu cha thamani kilichobakia kwao” amesema Schmeichel

Schmeichel ameyasema hayo wakati anajibu swali la mlinzi wa zamani wa Manchester City Micah Richards kuhusu mtazamo wake kwa United kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya.

United iliyo chini ya mkufunzi Ralf Rangnick watakuwa na kibarua kizito kwenye mchezo wa mtoano hatua ya 16 bora dhidi ya vijana wa Diego Simeone klabu ya Atletico Madrid katika dimba la Wanda Metropolitano nchini Hispania

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.