Chokoleti za KitiKat zaondolewa madukani kuhofiwa kuwa na vipande vya vyuma Afrika Kusini


Kampuni ya kutengeneza vyakula ya Nestlé imezirudisha kwa hiari baadhi ya chokoleti zake za KitkKat nchini Afrika Kusini baada ya kubaini kuwa zina vipande vya kioo wakati wa kukagua usalama.

Kampuni hiyo ilisema hakuna mteja aliyelalamika lakini hatua za kuzuia zinachukuliwa baada ya tatizo hilo kubaini.

Inasema kwa sasa inachunguza kitu gani hasa kilitokea katika chokoleti hizo kuona ikiwa chokoleti imeathirika, itabidi kuangalia nambari ya uzalishaji nyuma ya kifungashio.

Kwa mujibu wa BBC. Wateja ambao walikuwa wamenunua chokoleti zilizo na namba za utambulisho zilizoorodheshwa wameombwa kuzirejesha.

Utambulisho huo ni:

  • Nestlé KitKat 2 Finger Milk 36x20g UTZ MB yenye nambari ya uzalishaji “13590177” nyuma ya kifungashio”13600177″, “13620177”, “13630177”, “13640177”, “20010177” na “20100177” na
  • Mini Bag Milk 32x200g UTZ yenye nambari ya uzalishaji “20120177”, “20010177” “20020177” na “20030177”, “13620177”, “13600177” na “13610177” inayoonekana nyuma ya kifungashio.

Yeyote anayeshuku kuwa alitumia chocolate zenye utambulisho huo ameombwa kuonana na daktari. Nestlé inasema itaimarisha ukaguzi wake wa ubora ili kuhakikisha visa kama hivyo havitokei tena.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.