Simba wa Teranga watinga fainali AFCON, waichapa Burkina Faso 3-1
Miamba ya soka Barani Afrika Simba wa Teranga Senegal wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya AFCON baada ya kuifunga Burkina Faso kwa jumla ya magoli 3 – 1.
Magoli ya Senegal yakifungwa na wachezaji, Abdou Diallo 70′, Idrissa Gueye 76′ na Sadio Mane 87′ wakati lile la Burkina Faso likifungwa na Blati Toure 82′.
Waswahili husema aliyepewa kapewa, mbali na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali lakini pia kikosi cha Senegal kimetoa mchezaji bora wa mchezo huo ambaye ni Sadio Mane.
Hakuna maoni