Bilioni 2.4 Kuboresha Makumbusho Ya Taifa Nchini


Na Sixmund J. Begashe
Makumbusho ya Taifa nchini imepatiwa  shilingi Bilioni 2.4 ili iweze kutekeleza miradi 15 inayotekelezwa kwa fedha za Miradi ya Ustawu wa Nchi na Mapambano dhidi ya UVIKO 19, katika vituo vyake sita kikiwepo cha Azimio la Arusha Jijini Arusha.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga, alipo kuwa akifunga rasmi Maadhimisho ya mika 55 ya Adhimio la Arusha Jijini Arusha, sanjari na kuzindua Mradi mkubwa wa maboresho ya kituo cha Makumbusho ya Azimio la Arusha na Makumbusho ya Elimu Viumbe inayotekelezwa chini ya mpango wa Miradi ya Ustawi wa Nchi na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.

“Makumbusho ya Taifa ni moja ya Taasisi iliyoathirika sana kimapato kutokana na ugonjwa wa korona ambapo kumekuwa na upungufu mkubwa wa watalii wa ndani na nje ya nchi na kuathiri mapato ya Taasisi hii hivyo tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia viongozi wa Wizara yetu ya Maliasili na Utalii kwa kuipatia fedha Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kutekeleza miradi katika vituo sita na maeneo ya malikale sita”. Dkt Lwoga

Dkt Lwoga Licha ya kuupongeza uongozi wa Makumbusho ya Azimio la Arusha kwa ubunifu wa maadhimisho hayo ya siku muhimu ya storia ya nchi yetu, ameuagiza uongozi wa vituo vyote vya Makumbusho ya Taifa nchini kuhakikisha wanaongeza kasi ya ubunifu wa program zitakazo toa fursa kwa wananchi kujipatia elimu ya kutosha juu ya urithi wa kiutamaduni na Maikale uliohifadhiwa na Taasisi hiyo.

“Katika kituo cha Makumbusho ya Azimio la Arusha kuna mradi wa kuboresha maktaba na utengenezaji wa onesho la kudumu la Azimio la Arusha.  Katika Kituo cha Makumbusho ya Elimu Viumbe kuna mradi wa kukamilisha onesho la tembo kwa kuongeza wanyama watano wakubwa wanaovutia utalii wa wanyamapori, uwekaji wa maabara ya bailojia, uwekaji wa onesho la Reptilia, na uboreshaji wa stoo ya uhifadhi wa mikusanyo ya bailojia” Dkt Lwoga

Dkt Lwoga aliongeza kwa kuutaka uongozi wa vituo vyote vya Makumbusho ya Taifa nchini kuhakikisha unasimaia vyema fedha za mirahi hiyo 15 ili zilete mabadiliko yanayokusudiwa na wahakikishe miradi hiyo inakamilika kwa wakati uliopangwa.

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Azimio la Arusha Dkt Gwakisa Kamatula ameelezea umihimu wa utekelezaji wa miradi hiyo kuwa itasaidia kuvutia idadi kubwa ya watalii wa ndani na nje ya nchi pamoja na kuongezeka kwa mapato ya taasisi na Taifa kwa ujumla hivyo ameahidi  kuusimamia vyema mradi huo ili uweze kukamilika kwa haraka.

“Utekelezaji wa miradi hii ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo inaelekeza uboreshaji wa miundombinu na maonesho kwa ajili ya kukuza utalii na kuvutia watalii wa ndani na   nje ya nchi hivyo kukamilika kwa miradi hii kutawezesha vituo hivi kuwa na maonesho mazuri yanayovutia watalii wengi zaidi” Aliongeza Dkt Kamatula

Wakizungumzia maadhimisho hayo Wajasiria Mali wanafunzi na watu mbambali walioudhuria katika kilele hicho licha ya kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa jitihada kubwa inazofanya kuelimisha jamii na kufanya maboresho katika maonesho, wameshauri kasi ya kutoa elimu hiyo iongezeke kwani bado watanzania waliowengi hawana uwelewa wakutosha juu ya nini kimehifadhiwa kwenye Taasisi hiyo.

 “Nimefurahi sana kushiriki katika maadhimisho haya, sisi wajasiriamali tumepata fusra ya kuonesha kwa vitendo jamii matokeo bora ya ufanyaji kazi kwa faida ya taifa, maana hili lilikuwa ni moja ya azimio la Arusha, nawashauri akina mama, na wote kulienzi Azimio la Arusha kwa kufanya kazi kwa bidii ili kwa pamoja tulipeleke taifa letu mbele” Alisema Bi Anna Kombe

Maadhimisho hayo yamelenga kurithisha umma urithi wa historia  wenye misingi imara iliyosaidia na inaendelea kusaidia kusukuma maendeleo ya nchi misingi hiyo ni kama vile Umoja wa Kitaifa, Uwajibikaji, Udugu na Umoja, Utu, Uchapaji  kazi kwa faida ya wote

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.