Joao Cancelo ajitia kitanzi Manchester City
Manchester City wamethibitisha kuwa beki wao wa pembeni Joao Cancelo ametia saini mkataba mpya, utakaomfanya kusalia Etihad hadi mwaka 2027.
Mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika 2025 lakini City walikuwa na nia ya kumpa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mkataba ulioboreshwa zaidi kama zawadi kutokana na ubora wake, ambao umemfanya kuibuka kuwa mmoja ya wachezaji bora wa Ligi Kuu Soka nchini Uingereza.
Beki wa kulia, Cancelo ameng’ara pande zote za safu ya ulinzi ya City, akipachika mabao matatu na kutoa pasi nane za mabao kwa City hadi sasa msimu huu unaoendelea.
“Manchester City ni klabu kubwa, kwa hivyo nina furaha kubwa kusaini mkataba huu mpya,” alisema baada ya kusaini mkataba wake.
“Wachezaji wa City wana kila kitu wanachohitaji kufikia uwezo wao kamili, na vifaa vya kutosha vilivyokamilika, wachezaji wa kiwango cha kimataifa na meneja mwenye uwezo mkubwa ambaye hutusukuma kila siku. Hakuna mahali pazuri zaidi pa kucheza mpira wa miguu na ni raha kufanya kazi kama hapa.”
“Nina mengi ninayotaka kufikia kabla ya kufikia tamati katika kazi yangu ya soka, na Manchester City inanipa nafasi nzuri zaidi ya kutimiza matamanio yangu.
Mkurugenzi wa Soka Txiki Begiristain aliongeza: “Joao ni mchezaji mwenye uwezo wa hali ya juu. Anapenda mpira wa miguu kabisa na anajituma kila siku katika nia ya kuwa bora zaidi.”
Hakuna maoni