Rwanda yaboresha mitaa ya Kigali kuvutia watalii



Mtaa wa Biryogo ujulikanao tangu zama kama uswahilini ni kati ya maeneo takriban 100 yanayolengwa na serikalikuboreshwa miundo mbinu yake mbali mbali na mengineo kama kupandwa kwa miti ,maua na mtandao usiolipiwa.

Kwa mujibu wa Kigali John Gakuba kati kati ya barabarazilizopambwa kwa rangi mbali mbali mithili ya mwendo wa zigzag, wateja wameketi chini ya miavuli na wengine wamekaa barazani wakishiriki chai aina tofauti za vitafunwa .

Mitaa ya Biryogo ambayo imekuwa na kunawiriina historia ya kuwa chimbuko la jamii ya waislamu nchini Rwanda.


kuna wateja kutoka maeneo mbali mbali ya jiji wanakuja kuvinjari na kupata burudani, mkao kwa sehemu kubwa ukiambatana rika mahusiano ama maslahi.

Saa za jioni jioni ndipo watu wengi hukusanyika hasa katika mazingira haya huku vijana wa kujitolea waliovalina sare moja wakifuatilia utekelezaji wa masharti ya kuepuka maambukizi dhidi ya uviko-19.

Baadhi ya wamiliki wa nyumba kwenye mitaa hii wameelezea hofu kuhusu majaliwa yao kuishi katika jiji lenye kasi ya maedeleo na uwezekano wa kulihama jiji kutokana na kukosa uwezo wa kujenga ama kukarabati nyumba maskani yao.

TH

Lakini kwa upande mwingine wanajipa moyo kwani wamepewa vibali vya kukarabati nyumba zao ama vibanda vilivyochakaa kutoka kwa utawala wa manispaa ya jiji la Kigali.

Kulingana na afisa mwandamizi wa manispaa ya jiji la Kigali anayehusika na sanaa na uchoraji, Muhirwa Solange, manispaa ya Kigali imeshapata maeneo takriban mia jijini hapa ambapo kutawekwa maeneo ya vivutio vya watalii car free zone na mkaazi atawajibika kutumia nguvu zake za kifedha kukarabati mazingira yake kukiwemo maskani.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.